Chai FM

Chakula shuleni chatajwa kuwa chanzo uelewa wa wanafunzi

19 January 2024, 10:18 am

Ushirikiano mzuri baina ya wazazi na walimu umetajwa kuwa chachu ya ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi wa shule ya msingi.

Na Sabina Martin – RUNGWE,

Wazazi na walezi wilayani Rungwe wameshauriwa kushirikiana zaidi na walimu ili kuboresha maendeleo ya watoto kitaaluma na kiafya.

Akizungumza na Chai FM ofisini kwake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Madaraka wilayani Rungwe mkoani Mbeya Mwl. Gaspaer Idawa amesema suala la chakula shuleni ni sera ya serikali hivyo wazazi wanatakiwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

Aidha amesema kwamba mtoto akiwa na njaa ni hangamoto kwenye ufundishaji kwani kiwango chake cha uelewa huwa ni kidogo ukilinganisha na mtoto aliyeshiba.

Sauti ya Mwl Gasper kuhusu ushirikiano

Akizungumzia hali ya uandikishaji wa wanafunzi wa awali na darasa la kwanza Mwl. Idawa amesema kuwa shule ya msingi Madaraka wamevuka lengo kwani matarajio ilikua ni kuandikisha wanafunzi 80 kwa darasa la kwanza ambapo sasa wameandikisha wanafunzi 117 huku awali wakiwa na wanafunzi 167.

Sauti ya mwl. Gasper kuhusu uandikishaji

Kwa mujibu wa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2024 imeeleza kwamba serikali itaondoa vikwazo vinavyozuia mwanafunzi kuendelea na masomo na kukamilisha mzunguko wa elimu katika ngazi husika.