Chai FM

Wadau watakiwa kuibeba sekta ya elimu kwa wenye uhitaji

27 April 2022, 12:34 pm

Mkurugenzi wa Shule za Paradise na Patrick Mission ambaye ni mdau wa maendeleo Mkoa wa Mbeya ,Ndele Mwaselela ameguswa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji wapate elimu na kufungua milango ili wadau wengine waweze kujitokeza kusaidia wanafunzi wenye uhitaji .

Amesema kumekuwa na changamoto ya idadi kubwa ya wanafunzi wanapata fursa ya elimu ya ya juu na kukosa mikopo Serikalini  jambo ambalo linalowafaya kughaili kuendelea na masomo kwa mwaka husika.

Amesema hayo wakati wa Uzinduzi wa mfuko wa udhamini wa elimu ya juu kwa wanafunzi sita wa Chuo kikuu Kishiriki cha Katoliki  Mbeya (CUCOM) ulianzishwa na mdau huyo wa elimu .

Naye Makamu  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mt Augustino (SAUT) Prof .Coster Ricky  Mahalu amesema changamoto ya kukosa  mikopo ya elimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu imewafanya waweke  mikakati ya kuanzisha mfuko kwa ajili ya kuendeleza wanafunzi wenye uhitaji wanaotoka familia zisizojiweza.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa kanisa katoriki na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec)Gervas Nyaisonga amesema viongozi wa vyuo vikuu vya kanisa wasisite kuwashirikisha wadau kwani lengo ni kupaza sauti za wenye uhitaji.

Mwanafunzi aliyepata udhamini wa masomo ,Grady Sanga ,amesema wamekuwa wanakwama kuendelea na masomo kutokana na kukosa mikopo ya elimu ya juu ambapo kwa sasa watanufaika na ufadhili huo na kuhitimu elimu ya juu pasipo changamoto ya ada.