Chai FM

Ujenzi daraja mto Lufilyo mkombozi kwa wakazi wa Luteba, Lufilyo

18 August 2023, 12:21 pm

Na Lennox Mwamakula

Wananchi wa kata ya Luteba Halmashauri ya Busokelo wameonesha kufurahishwa na ujenzi wa daraja ambalo linaunganisha kata ya Luteba na Lufilyo.

Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Lulasi kata ya Luteba Mbunge wa Jimbo la Busokelo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete amesema daraja hilo ni mkombozi kwa wananchi wa kata hiyo kwani litaongeza uchumi kwa wananchi.

Hata hivyo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasan kwa kutoa fedha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mia saba arobaini na moja(mil. 741) ambazo zimewezesha ujenzi huo kukamilika.

Sauti ya naibu waziri wa uchukuzi

Naibu Waziri wa Uchukuzi na mbunge wa jimbo la Busokelo Mh. Fredy Atupele Mwakibete katikati, wakielekea kukagua ujenzi wa daraja linalounganisha kata ya Lufilyo na Luteba

Abel Masaba ni Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Rungwe amesema ujenzi wa daraja hilo ulianza mwezi Oktoba mwaka jana na umekamilika Juni mwaka huu huku ukigharimu zaidi ya shilingi million 741.

Sauti ya kaimu meneja wa tarura

Kwa upande wake diwani wa kata ya Luteba Ayubu Mwalubona amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mbunge kwa kufanikisha ujenzi wa daraja hilo.

Sauti ya diwani wa kata ya Luteba

Nao baadhi ya wananchi wa kata ya Luteba Halmashauri ya Busokelo wameonesha kufurahishwa na ujenzi wa daraja hilo ambalo litawarahisishia katika usafirishaji wa mazao mbalimbali.

vox pop wananchi.