Chai FM

Dsw kuimarisha mifumo ya kuzuia ukatili wa kijinsia

25 April 2024, 1:49 am

ili kukabiliana na vitendo ya ukatili wa kijinsia kwa watoto jamii imetakiwa kuwa mstari wa mbele kutoa tarifa kwenye vyombo vya kisheria.

MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Shirika lisilo la kiserikali la DSW Tanzania linalojihusisha na masuala ya maendeleo Kwa vijana hapa nchini April 24 mwaka 2024 limewakutanisha wadau mbalimbali na kufanya kikao Cha kuhimarisha mifumo ya kuzuia ukatili wa kijinsia.

Kikao hicho Cha kuimarisha mifumo ya kuzuia vitendo vya ukatili kimefanyika kwenye ukumbi wa meya uliopo kwenye jingo la  Halmashauri ya jiji la mbeya lengo ikiwa ni kutoa elimu juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na vijana pamoja na kuangalia sera,sheria,mipango sambamba na mikakati iliyopo.

mratibu wa mradi Bi,Mariam Abraham akielezea namna mradi unavyofanya kazi

Akifungua kikao hicho mkurugenzi wa shirika hilo peter luwaga amesema shirika la DSW linatekeleza mradi wa SAFA wenge lengo la kuwawezesha vijana kuiboresha maisha Yao katika nyanja za afya,stadi za maisha,elimu ya ufundi,kilimo na ajira,elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na elimu ya afya ya uzazi.

wadau wa kupinga vitendo vya ukatili wakimsililiza mmja wa wawezeshaji akitoa elimu[picha na Lennox Mwamakula]

sauti ya mkurugenzi wa Dsw

Kwa upande wake mratibu wa mradi Mariam Abraham amesema kikao hicho kimewashirikisha wadau mbalimbali kama vile walimu wa shule za secondary kwani wao kwa muda wingi wanakuwa na vijana hivyo elimu watakayp ipata itasaidia kufikia malengo ya kukabiliana na vitendo vya kupinga ukatili wa kijinsia na kuwa na jamii iliyo salama

Afisa mradi shirika Dsw Shamsa Khalfan akizungumzia juu ya vitendo vya ukatili [picha na Lennox Mwamakua]

sauti ya mratibu wa shirika la Dsw

Hata hivyo naye afisa mradi mkoa wa Mbeya Shamsa Khalfan amesema asilimia 67  ya watoto wanatumia mitandao ya kijamii wadau wa kupinga ukatili ni bora kuendelea kuwalinda na kuwaelimisha juu ya madhara ya matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuweza kujenga kizazi bora kwa manufaa ya baadaye

Sauti ya afisa mradi

Aidha naye afisa maendeleo ya jamii mwandamizi kutoka Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Bw,Victor Rugalabamu amesema ukosefu wa elimu kwa baadhi ya wazazi juu ya namna ya utoaji adhabu kwa watoto kunachangia kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa watoto,na amesema kwa mujibu wa takwimu zilizofanywa na shirika la kuhudunia watoto duniani UNICEF mwaka 2015 takribani asilimia sitini vitendo vya ukatili wamefanyiwa watoto majumbani.

Sauti ya afisa maendeleo mwandamizi