Chai FM

Wananchi wafurahia ujenzi wa barabara ya katumba-mwakaleli

30 April 2024, 6:59 pm

serikali imeendelea kuboresha miundombiu ya barabara kwa dhumuni ya kuunganisha halmashauri zote nchini ili kuweza kufikika kwa urahisi

wananchi wakiwa kwenye furaha baada ya mkandarasi kukabidhiwa barabara ili anze kujenga [picha na lennox mwamakula]

RUNGWE-MBEYA

Na lennox Mwamakula

Serikali imetenga fedha Kiasi cha shilingi Bilion 87 kwaajili ya ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha  Lami kutoka Katumba Mpaka Lupaso yenye urefu wa KM 35.5 na Mbaka-Kibanja KM20.7 leo tarehe 30.4. 2024.

Hafla hiyo ya kukabidhi na kutambulisha mradi huo imefanyika chini ya mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh, Jaffar Hanniu eneo la katumba mbele ya wananchi na kampuni iliyo kabidhiwa ujenzi wa barabara hiyo ni kampuni ya China Road Construction

mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar hanniu akizungumza na wananchi mji wa katumba kwenye hafla ya makabidhiano ya barbara picha na lennox mwamakula

Hanniu amesema kutokana na kilio cha wananchi cha muda mrefu serikali imetafuta kampuni hiyo ili kuweza kufanikisha ujenzi wa barabara hiyo na wananchi waweze kusafirisha mazao yao na kupata soko la uwakika 

sauti ya mkuu wa wilaya 1

Mhe.Haniu amewaomba wakazi wa maeneo yote mradi utapotekelezwa kuendelea kutoa ushirikiano huku wakijiepusha na vitendo vvya uhujumu wa mali za Mradi wa barabara.

Aidha amewaagiza wakazi wote waliojenga katika hifadhi ya barabara kuhakikisha wanaondoa miundombinu yao ili kufanikisha mradi kwa uharaka na kuiepushia gharama serikali ya kumlipa Mkandarasi baada ya kuchelewesha uanzishwaji wa mradi.

sauti ya mkuu wa wilaya 2

Serikali imetoa siku 60 kuanzia leo kuhakikisha kila mkazi anaondoa mali zake katika hifadhi ya umbali wa mita 22.5 kila upande wa barabara.

Hata hivyo amwagiza Wakala wa barabara nchni (TANROAD) Kwa kushirikiana na Mkandarasi kuhakikisha wanatoa ajira kwa vijana waliopo katika vijiji Vya jirani ikiwa ni sehemu ya kuwaongezea kipato na ulinzi wa mradi

Mkandarasi wa kampuni ya china Road Construction wakiwa kwenye makabihiano ya barabara ya katumba hadi lupaso

Katika hatua nyingine Mhe.Haniu ametoa maelekezo kwa wakazi wa wilaya ya Rungwe kuendelea kuchukua tahadhari kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo miundombinu mbalimbali imeharibika na kuwa Serikali inaendelea kuhakikisha mawasiliano ya barabara yanafunguka ili wananchi waendelee kunufaika na matunda ya nchi yao.

sauti ya mkuu wa wilaya 3

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya busokelo Anyosisye Njobelo ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia suluhu Hasani kwakuendelea kutoa fedha kwajili  ya kuwaondolea wananchi changamoto ya ubofu wa miundombinu ya Barabara.

sauti ya Mwenyekiti wa halmashauri