Chai FM

Zaidi ya milioni 3 kukarabati shule Rungwe

8 March 2024, 11:24 am

Katibu wa mbunge mwenye suti ya dark blue Bw. Gabriel Mwakagenda akimpa mkono mwenyekiti wa kijiji cha Iringa Festo Mwakajisi

Shule ya msingi Katumba one ni shule iliyojengwa miaka 50 iliyopita na kutumika bila kufanyiwa ukarabati wowote, hatimaye sasa inakwenda kukarabatiwa kwa ufadhili wa mbunge.

Na Bahati Obel

Mbunge wa jimbo la Rungwe Anton Mwantona amekabidhi msaada wa bati 108 zenye thamani Ya   shilingi 3,780,000 katika shule ya msingi katumba one iliyopo kata ya  Ibigh kwa ajili ya umaliziaji wa majengo mawili ya madarasa yaliyofikia hatua ya kupaua.

Msaada huo umekabidhiwa na katibu wa Mbunge ndugu Gabriel Mwakagenda amewataka viongozi wa shule hiyo kutosita kuomba msaada wa cement watakapo maliza kupauwa ili wanafumzi waweze kusoma katika mazingira mazuri.

Sauti ya mbunge wa Rungwe

wakizungumza mara baada ya kupokea msaada huo viongozi wa chama cha mapinduzi kata ya ibigh wakiongozwa na mwenyekiti wao  Itika Mkoba wamemshukuru mbunge wa jimbo la Rungwe kwa kuendelea kutimiza ahadi yake katika kata hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa mabati yatakayo tumika kuezeka majengo mawili ya madarasa katika shule ya msingi katumba one.

Sauti ya viongozi wa CCM Rungwe

Kwa upande wao viongozi wa shule ikiwa ni pamoja na mwalim mkuu wa shule hiyo bi Shirima na mwenyekiti wa kamati ya shule Lusekelo Mwakyambiki mbali na kutoa shukrani zao kwa wananchi na mbunge wameeleza kuwa bado kumekuwa na changamoto ya vyumba viwili vya madarasa na hivyo kuomba kufikishiwa salam zao kwa mbunge wa jimbo hilo.

Sauti za viongozi wa shule

Katika Hatua Za Awali Mbunge Mwantona Alikabidhi Mifuko 150 Ya Saruji kwa ajili ya hatua Za mwanzo za ujenzi wa vyumba hivyo vya Madarasa.