Chai FM

Chakula shuleni chachu ya ufaulu Rungwe

14 March 2024, 8:08 am

Katibu tawala wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Ally Kiumwa akizungumza na wajumbe kwenye kikao cha Tathimini juu ya lishe [picha na Lennox mwamakula]

Imeelezwa kuwa asilimia 93.7 ya wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo yao ni wale wanaokula chakula cha mchana shuleni

Na Lennox Mwamakula – RUNGWE

Wazazi na walezi wilayani Rungwe mkoani Mbeya wameshauriwa kuchangia fedha ya chakula shuleni Kwani Kunasaidia ufaulu na kuimamarisha akili Kwa mtoto.

Kauli hiyo imetolewa na afisa lishe wa wilaya Bi,Halima Kameta kwenye kikao Cha tathimini ya lishe kilichofanyika kwenye ukumbi wa John Mwankenja halmashauri ya Rungwe ambapo amesema asilimia 93.7 ni wanafunzi wanao pata chakula wawapo shuleni.

saut ya afisa lishe wa wilaya ya Rungwe 1

Bi kameta ameongeza kuwa ulaji wa chakula shuleni pia umepunguza idadi ya watoto wanaotoroka shule badala yake imejenga mahusiano mazuri baina ya watoto na walimu wao.

Wajumbe walioshiriki kwenye kikao cha lishe [picha na Lennox mwamakula]

sauti ya afisa lishe wa wilaya 2

Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria kikao hicho amesema kuwa ipo haja ya halmashauri kutunga sheria ndogo itakayosaidia wazazi kushiriki zoezi la uchangiaji wa chakula shuleni.

sauti ya mjumbe

Kwa upande wake mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni katibu Tawala wilaya ya Rungwe Bw. Ally Kiumwa ameagiza wajumbe wote kila mmoja kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia kwamba ajenda ya lishe ni ya kudumu hivyoinapaswa kutekelezwa kwa weledi.

sauti ya katibu tawala ally kiumwa