Chai FM

Wananchi Tukuyu walilia matuta kupunguza ajali za barabarani

16 October 2023, 11:48 am

Na Sabina Martin Rungwe-Mbeya
Kufuatia uwepo wa ajali za mara kwa mara katika eneo la ushirika mji mdogo wa Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mbeya wananchi wa eneo hilo wameiomba serikali kuweka matuta katika eneo hilo.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na chai FM wamesema kuwa baada ya kuondolewa tuta lililokuwepo hapo awali imekuwa sababu ya ajali za mara kwa mara katika eneo hilo.

Aidha wananchi hao wamesema kuwa baadhi ya madereva hawazingatii alama za barabarani hali inayohatarisha usalama wa watumiaji wa barabara.

Sauti ya wananchi ushirika

Akizungumza na Chai Fm Meneja wa TANROADS mkoa wa Mbeya Matari Masige amewataka watumiaji wa barabara hususani madereva kuwa waaminifu kwenye matumizi sahihi ya alama za usalama barabarani.

Sauti ya Matari masige meneja wa TANROAD mkoa wa Mbeya

Katika hatua nyingine amewataka wananchi kuandika barua ya kuomba kujengwa tuta kwenye eneo hilo kutokana na ulazima wake.

Sauti ya Matari masige meneja wa TANROAD mkoa wa Mbeya 2

Kilio cha wananchi wa eneo la ushirika mji mdogo wa Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mkoani Mbeya kimekuja kufuatia kuondolewa kwa tuta lililokuwepo awali katika eneo hilo la barabara kuu ya Uyole – Malawi.