Chai FM

Miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bil 2.427 yapitiwa na Mwenge wa Uhuru Rungwe

8 September 2023, 10:11 am

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jafari Hanniu ametakiwa kusimamia vizuri mradi wa maji wa Ikuti –lyenje ili mradi huo ukamilike kwa muda ulioyo pangwa .

Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ndg. ABDALLAR KAIM kwenye chanzo cha maji cha genge uliopo kata ya Ikuti wilayani Rungwe mkoani Mbeya mradi ambao unakwenda kutatua changamoto ya maji ndani ya kata hiyo pamoja na kata za jirani.

Sauti ya kiongozi wa mwenge 1……………………

Mkuu wa wilaya ya Rungwe wakwanza kushoto akipokea maelekezo kutoka kwa kiongozi wa mwenge wa uhuru kitaifa

Kwa mujibu wa taarifa ya mradi huo wa maji ulianza kutekelezwa march 1. 2022 ambapo ulitarajiwa kukamilika septemba 30. 2022 huku ikibainishwa changamoto zilizokwamisha mradi kukamilika kwa wakati ni ucheleweshwaji wa vifaa kama vile bomba na vifaa vingine vya ujenzi.

Taarifa ya mradi 1………………………

Hata hivyo risala imebainisha kuwa mradi huo unahusisha ujenzi wa matenki mawili ya kuhifadhia maji pamoja na vituo 44 vya kutolea maji kwa wananchi ambapo mradi huo umefikia asilimia 55 ya utekelezaji wake na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi februari 2024.

Taarifa ya mradi 2………..

Kutokana na mwananchi wa eneo hilo kutoa eneo kwaajili ya ujenzi wa Tanki la maji bila kudai fidia kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa amemwagiza mkuu wa wilaya ya Rungwe kuhakikisha mwananchi hyu kupelekewa maji safi na salama nyumbani kwake kutokana na uzalendo aliyo uonyesha.

Sauti ya agizo…………

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya ya Rungwe amepokea magizo hayo na hilo na amesema mwananchi huyo atapatiwa maji ya bomba ndani ya mwezi wa kumi mwaka huu.

DC Rungwe………

Sambamba na hilo mwenge wa uhuru wilayani Rungwe umekagua miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa shule mpya ya msingi kibumbe, mradi  wa jengo la dharura katika hospitali ya wilaya pamoja na uwekaji wa jiwe la msigingi kwenye stendi ya daladala  Tukuyu mjini.