Chai FM

Watumiaji wa barabara watakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani

18 March 2022, 9:19 am

RUNGWE

Na Lennox Mwamakula

Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani wilayani Rungwe mkoani Mbeya FELIX KAKOLANYA amewataka waendesha  vyombo vya moto kufuata sheria za barabarani wanapo tumia vyombo hivyo.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungunza na madereva pamoja na watumiaji wengine wa barabara kwa njia  ya redio kwenye kipindi cha amka na chai FM amesema waendesha vyombo vya moto wamekuwa na Tabia ya uvunjaji wa sheria wakati  elimu inatolewa mara kwa mara kwa wamiliki, madereva na abiria.

Hata hivyo Kakolanya ameagiza waendesha vyombo vya moto kukata stika kwa lengo la kutambulika kwa vyombo vya moto usalama wake kwa ambaye atakaidi hatua kali itachukuliwa dhidi yake.

Akizungumzia suala la madereva kuwa na tabia ya kupandisha nauli amesema ni kinyume na utaratibu kwani kuna mamlaka zinazo husika hivyo amewataka madereva wote Wilayani Rungwe kusubiri tamko kutoka mamlaka hiyo.