Chai FM

Ujio wa vituo vya afya kuwa mkombozi kwa wananchi

7 October 2023, 8:11 am

kituo cha afya ndanto {picha na lennox mwamakula}

wananchi wafurahia huduma ya afya wilaya rungwe kutokana na kuondokana na changamoto ya muda mrefu.

RUNGWE-MBEYA

Na lennox mwamakula

Jumla ya wakazi elfu kumi na nanene wanaenda kunufaika na huduma ya afya  pindi ujenzi wa jingo la mama na mtoto litakapo kamilika kwenye kituo cha afya  kata ya ndanto utakapo kamilika

Samwel Mwinuka ni diwani wa kata  ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na mwanahabari wetu alipotembelea kata hiyo na kujionea shughuli za maendeleo hasa ujenzi wa kituo cha afya kilichojengwa  kijiji cha cha Ntokela.

Amesema uwepo wa kituo cha afya ndani ya kata hiyo kumesaidia kuondolea adha ya kutembea umbali mrefu ya kufuata huduma hiyo kwani awali wananchi walikuwa wakifuata huduma hiyo katka hospitali ya mission igogwe na hosptali ya wilaya Makandana

Sauti ya mwinuka  1

Aidha  mwinuka amewaomba wananchi wa kata hiyo kuendelea kujitoa kwenye shughuli za maendeleo kwani bado changamoto bado zipo kama vile uboreshwaji wa miundombinu ya barabara,kwani serikali ni sikivu suala la Barabara utafanyika kadili fedha zitakapo patikana

SAUTI  YA MWINUKA 2

Kwa upande wake Sara  osiah mkazi wa kata hiyo imeshukuru serikali kwa kuwasogezea huduma ya afya kwani amesema kumewasaidia kuondokana na adha ya kufuata huduma hiyo kwenye kata za jirani ambapo huduma zilikuwa zikipatikana

Sauti ya sara