

11 February 2025, 11:24 am
RUNGWE-MBEYA
Mikopo ya serikali inawasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi kwa ngazi ya familia na kuinua chumi wa halmashauri kwa ujumla.
Na Lennox Mwamakula
Zaidi ya shilingi Milioni 177 zimetolewa na Halmashauri ya wilaya ya Busokelo kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ikiwa kwa awamu ya kwanza
Zoezi la uzinduaji wa utoaji wa mikopo kwa halmashauri ya busokelo limefanyika kata ya Ntaba mbele ya mwenyekiti ya halmashauri mh, Anyosisye Njobelo ambaye amewasihi wanufaika wa mikopo hiyo kwenda kuzifanyia kazi kwa malengo walio jiwekea
sauti ya mwenyekiti wa halmashauri
Awali akisoma taarifa ya mikopo kaimu mkuu wa division ya maendeleo jamii wilaya Busokelo Ndg,John Kipingili amesema kabla ya utoaji wa mikopo hatua mbalimbali zilichukuliwa ikiwa ni utoaji wa elimu kwenye vikundi pamoja na kamati za mikopo ili kuvitambua vikundi vilivivyo kidhi vigezo
sauti ya afisa maendeleo 1
Hata hivyo kipingili amewaomba wananchi waliokosa kupata mikopo awamu ya kwanza waendele kuboresha taarifa zao na kuwatumia maafisa mikopo ngazi ya kata ili kupata elimu kujua vigezo vinavyo takiwa kwa wanufaika
sauti ya afisa maendeleo 2
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Busokelo Dr mwinyi omary mwinyi amewaomba wananchi kujitokeza kujisajili ili waweze kupatiwa fendha ili waweze kundelea kufanya shughuli zao za kujikwamua kiuchumi
wanufaika wa mikopo halmashauri ya busokelo
sauti ya mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Busokelo
Naye katibu tawala wa wilaya ya Rungwe Ndg Ally Kiumwa amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa kikundi kitakacho sita kurejesha fedha hizo kwa muda uliopangwa
sauti ya katibu tawala
Kwa upande wao wanufaika wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwapatia mkopo huo kwani wamesema fedha hizo zinakwenda kuwainua kiuchumi kwenye familia zao
sauti ya wanufaika