Chai FM

Jamii ijitokeza kupata matibabu ugonjwa wa Ukoma

29 January 2022, 7:26 am

RUNGWE-MBEYA

Jamii imetakiwa kujitokeza kupata matibabu pindi waonapo dalili za ugonjwa wa Ukoma hali itakayosaidia kuzuia maambukizi kwa wengine.

Rai hiyo imetolewa na Mratibu wa kifua kikuu na Ukoma wilayani Rungwe Daktari Emmanuel Asukile alipokuwa akizungumzia kuelekea maadhimisho ya siku ya ukoma dunia ambayo hufanyika tarehe  30  mwezi 1 .

Mratibu wa kifua kikuu na Ukoma wilayani Rungwe Daktari Emmanuel Asukile amesema maadhimisho haya ufanyika na yanasaidia kufikisha elimu kwa jamii na kuongeza ufahamu kuhusu ugonjwa wa ukoma ambapo lengo la wizara ni kumaliza tatizo hili ifikapo 2030.

Ameongeza kuwa ugonjwa huu uenezwa kwa njia ya hewa ambapo vimelea vya ukoma vinapokuwa kwenye hewa na mtu asiye na maambukizi akapita eneo hilo kuna uwezekano wa kuapata maambukizi kwa haraka.

picha ya mgonjwa wa ukoma namna alivyopata athari katika ngozi

Kuelekea katika maadhimisho ya Ukoma duniani tarehe 30 mwezi huu yanaenda na kaulimbiu isemayo tuungane kulinda utu wa  watu wanaougua  ukoma.