Chai FM

Transfoma yahatarisha usalama wa wafanyabiashara Rungwe

21 March 2024, 6:15 pm

Ili kuhakikisha shughuli za kibinadamu kufanyika, binadamu anatakiwa kuweka mazingira ya kazi yake salama.

Na lennox Mwamakula

Wafanyabiashara wa ndizi kwenye soko la Mabonde lililopo kata ya Msasani wilayani Rungwe wameiomba serikali kuwaboreshea soko hilo.

Baadhi ya wafanyabiashara wakiendelea na shughili zao chini ya Transfoma. Picha na Lennox Mwamakula

Kauli hiyo wameitoa walipokuwa wakizungumza na Chai Fm, wamesema baada ya kuhamishwa walipokuwa awali na kupelekwa eneo jipya kumekuwa na changamoto nyingi  kama vile miundombinu ya eneo la kukusanyia ndizi  kutokuwa rafiki, barabara kutopitika kwa urahisi pamoja na taka kurundikana sehemu moja kwa muda mrefu bila kuondolewa.

Hata hivyo wafanyabiashara hao wamesema kutokana na ufinyu wa eneo hilo pia wanamwomba Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe kuwaondolea transfoma iliyopo katikati ya soko kwani wamesema inahatarisha usalama wa wafanyabishara hao.

Sauti ya wafanyabishara 1

Aidha wanunuzi wa ndizi wamelalamikia tabia zinazojitokeza kwenye soko hilo kwa baadhi yao kutokuwa waaminifu kwa kuwaibia wenzao ndizi kitendo ambacho kinawakatisha tamaa wafanyabishara wanaotoka mikoa mingine na nchi jirani kama Malawi na Zambia kuendelea kuja kununua ndizi kwenye soko hilo.

Hali ilivyo kwenye soko la ndizi mabonde [picha na lennox mwamakula
Sauti ya wafanyabiashara 2

Kwa upande wake katibu wa soko hilo la  ndizi Mabonde Bi Elika  kutokana na malalamiko hayo juu ya suala la watu wachache wenye tabia za kukwamisha juhudi za wenzao na amesema kuhusu suala la ni nani anapaswa kulinda  ndizi kabla azijasafirishwa

sauti ya katibu wa soko