Chai FM

26 May 2022, 9:49 am

RUNGWE-MBEYA

NA:LETHISIA SHIMBI

Jamii wilayani Rungwe mkoani Mbeya imetakiwa kuachana na mtazamo hasi kuhusu watu wenye ulemavu badala yake wametakiwa kujumuika kwa pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali.

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa shirika la TRAIDCRAFT EXCHARGE Ndg Ledis Kigala kwenye  mkutano na wananchi uliofanyika katika ofisi za CCM  kijiji cha Nsongola kata ya Bujela ambapo amesema kuwa watu wenye ulemavu wamekuwa wakibaguliwa katika jamii kitendo ambacho kinapelekea watu hao kukosa sauti katika jamii.

Aidha amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakitumia majina yasiyostahili kuwaita watu wenye ulemavu kwa mfano kipofu ,zeruzeru,badala ya kusema mtu asiyeona ,au albino.

naye mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu(CHAWATA) Ndg  EMU KASOKE ameitaka jamii kutokuwa na tabia za kuwatenga bali kuwapa  nafasi katika jamii na wana haki  kama watu wengine.

kwa upande VERONIKA DANIEL Afisa usitawi wa jamii wilayani Rungwe amekemea vikali kitendo cha ubaguzi kwa watu wenye ulemavu na amesema kuwa endapo itabainika jamii au mzazi anambagua mtu mwenye ulemavu na kutompa haki yake jamii itoe  taarifa kwenye ofisi za ustawi na jeshi la polisi kupitia dawati  la jinsia ili hatua kali zichukuliwe

TRAIDCRAFT EXCHARGE ni shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na mambo mbalimbali ikiwemo kuelimisha jamii juu ya kubadilisha mitazamo hasi kwa watu wenye ulemavu.