Chai FM

Wananchi watakiwa kuzingatia lishe bora kwa watoto

31 January 2024, 1:35 pm

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki warsha ya lishe [Picha na Sabina Martin]

Jamii imeshauriwa kuzingatia lishe bora kwa watoto ili kujenga mwili pamoja na kuimarisha afya ya akili kwa ujumla.

Na Sabina Martin

Wanafunzi waliopatiwa elimu ya lishe bora halmashauri ya wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa kuwa mabalozi wa lishe katika jamii ili kuwa na jamii ambayo watu wake ni wenye afya bora.

Akizungumza katika uzinduzi wa warsha ya utoaji elimu ya lishe iliyokutanisha shirika lisilo la kiserikali la Asante Afrika Foundation, wataalam wa afya na lishe wilaya, walimu na wanafunzi wa baadhi ya shule za secondary wilayani hapa katibu tawala wilaya ya Rungwe Bw. Ally kiumwa amesema kwamba maendeleo mazuri ya wanafunzi hao shuleni ni matokeo ya lishe bora.

Katibu tawala wa wilaya akitoa neno kwenye warsha mbele ya washiriki

sauti ya katibu tawala wa wilaya ya Rungwe

Baadhi ya walimu waliopatiwa mafunzo hayo wametoa rai kwa wazazi kupitia watoto wao kuzingatia mpangilio wa vyakula kwa kutumia vyakula vinavyopatikana  katika maeneo yao.

sauti za walimu walioshiriki warsha

Maria Ngilisho ni afisa lishe mtafiti mwandamizi kutoka taasisi ya chakula na lishe Tanzania chini ya wizara ya Afya amesema kwamba lengo la kutoa elimu ya lishe ni kubainisha makundi sita ya vyakula ili kuhamasisha jamii kuzingatia mlo kamili.

sauti za afisa lishe mwandamizi

Kwa upande wake afisa kilimo mwandamizi kutokea wizara ya kilimo Beatrice Ntoga amesema kuna uhusiano mkubwa kati ya kilimo na lishe kwani asilimia kubwa ya mahitaji ya lishe ni chakula kitokanacho na mazao mbalimbali yanayotegemea udongo.

sauti ya afisa kilimo mwandamizi