Chai FM

Uwt wainuana kiuchumi mkoa wa Mbeya

26 December 2023, 9:51 am

katika kuhakikisha wanawake wanajikwamua kichumi jumuiya ya wanawake ya chama cha mapinduzi mkoa wa mbeya wanatarajia kuanzisha saccos.

RUNGWE-MBEYA

Mwenyekiti wa chanma cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya Patric Mwalunenge ametoa ushauri kwa Jumuiya ya  umoja Tanzania [UWT] mkoa wa Mbeya kuanzisha SACCOS ili waweze kuinuana kiuchumi.

Kauli hiyo ameitoa kwenye Hafla ya kuwapongeza wanawake wa chama cha Mapindunzi mkoa wa Mbeya  kwakuwa  wajasiriamali  wazuri na kuinua uchumi wa familia iliyoandaliwa na Mbunge wa viti maalum Mkoa wa mbeya ambaye pia ni Naibu waziri wa maji Maryprica Mahundi iliyofanyika kwenye fukwe za ziwa nyasa zilizopo wilyani kyela  siku ya ijumaa ya Tarehe 22 disemba mwaka 2023

Mh,maryprisca mahundi akiongea na uwt mkoa wa mbeya [Picha na lennox Mwamakula]

Sauti ya mh,maaryprisca mahundi

Wakiwa kwenye hafla hiyo ya kupongezana wanawake hao walipata nafasi ya kueleza shughuli wanazo zifanya za kujiingizia kipato baada ya mh, Mahundi kuwawezesha mtaji mwaka 2022 wamesema kwasasa wamekuwa wajasirialiamali na wanasomesha familia zao

uwt wakiwa kwenye fukwe za ziwa nyasa wilayani kyela

sauti za wajasiriamali

Kwa upande wake mgeni Rasmi kwenye hafla hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha mapindunzi mkoa wa Mbeya  Patric Mwalunenge amempongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya maryprsca Mahundi  kwakuwa na wazo la kuinuana kiuchumi kwa wanawake na kumuomba kuazisha SACCOS na kuweka utaratibu wa kuweza kukopesheka

Mwenyekiti wa chama cha mapindunzi mkoa wa mbeya mh, Patric Mwalunenge apowasili fukwe za ziwa nyasa

sauti ya mwenyekiti

Naye Mkuu wa wilaya ya kyela Mh,Jjosephine Manase ametumia fursa hiyo kwa kuwaomba wawekezaji kufika ndani ya wilaya hiyo kwani amesema kuna fursa nyingi za uwekezaji kama vile kilimo,uvuvi pamoja na maeneo ya  kujenga hoteli kwenye mwambao wa ziwa nyasa

sauti ya mkuu wa wilaya ya kyela

Jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi mkoa wa mbeya wamemshukuru Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Mbeya kwa jitihata anazozifanya kwao kwani wamesma kwasasa wamejikwamua kiuchumi na wanategemewa kwenye familia zao

sauti za uwt