Chai FM

Madiwani msiwe chanzo cha migogoro Rungwe

1 May 2026, 9:50 am

tuilinde amani ya nchi kuanzia ngazi ya familia na taifa kwa ujumla

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Madiwani wilayani Rungwe wameombwa kupitia taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali ili kuweza kurekebisha makosa na changamoto zilizo  bainishwa kwenye taarifa hiyo kwa lengo ya kuendelea kupata hati safi.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh, Jaffar Hanniu kwenye kikao cha Baraza la madiwani kwa kipindi cha Robo ya Tatu kuanzia January hadi March 2026 kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe wa john Mwankenja amesema madiwani kuendelea kukusanya mapato ya ndani ndiyo msingi kuwezesha mipango ya maendeleo ya wilaya

Sauti ya DC 1

Mh, Hanniu  amesema kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha amewaomba madiwani kutoa elimu kwa wananchi namna ya kukabiliana  na mmomoyoko wa ardhi kwa kupanda miti ili kuweza kudhibiti madhara yanayoweza kujitokeza.

Sauti ya DC 2

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Rungwe Mh, Gabriel Mwakagenda amepongeza madiwani kwa ushirikiano wanaounyesha na kuwaomba kuendelea kudumisha amani kwenye kata na wasiwe chanzo cha kuanzisha migogoro ndani ya maeneo yao kutakwamisha maendeleo ya wilaya na Taifa kwa ujumla

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri

Pia Mwakagenda amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri kuandaa utaratibu  ndani ya siku saba kwajili ya kamati ya fedha ili kupitia mradi ambao baraza limeagiza

Sauti   ya maagizo

Renatus Mchau ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe ameliakikishia baraza kuwa yale yote yaliyo agizwa yanaenda kutekelezwa ili malengo ya halmashauri yaweze kufikiwa

Sauti ya mkurugenzi mtendaji