Chai FM

Mseleleko wawaponza vijana VVU

21 October 2021, 12:09 pm

RUNGWE

Vijana wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wameelezea sababu zinazo pelekea baadhi ya vijana kupata maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kutokana na tafiti zilizotolewa na tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids).

Tafiti hizo za mwaka 2020 zimebainisha kuwa vijana kati ya umri wa miaka 14 hadi 25 ni kundi lililo hatarini katika maambikizi mapya  ya  Virusi vya Ukimwi ukilinganisha na makundi mengine.

Radio Chai imepata nafasi ya kuzungumza na  vijana Wilayani Rungwe wamesema kuwa baadhi yao wamekuwa na utaratibu wa kuto pima afya zao mara kwa mara kitu kinacho sababisha vijana hao kuishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi pasipo kujitambua.

Aidha wameongeza sababu nyingine inayo sababisha vijana kupata maambukizi haya ni pamoja na wazazi kutokuwa na kawaida ya kuwapa elimu kuhusiana na hali ya woga au aibu pasipo kujua nyakati za sasa ni utandawazi ambapo vijana hayo wanajifunza mambo mengi kutoka katika mitandao ya kijamii.

Gwakisa Kamoma na Paul Alex wameelezea sababu zinazo pelekea jamii hususani vijana kutokuwa na kawaida ya kupima afya zao mara kwa mara sababu kubwa ni hofu ya kujua afya zao.

Sambamba na hayo wameelezea umuhimu wa kupima afya zao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua mapema endapo watatambulika na ugonjwa huo huku wakishauri vijana   kuacha  ngono zembe badala yake watumie kinga ili kuweka kutimiza malengo yao.