Chai FM

Vitendo vya ukatili kwa watoto kukomeshwa Rungwe

16 June 2024, 8:45 pm

wadau wa kupinga vitendo vya ukatili kushirikiana na wazazi kutokomeza vitendo vya vya ukatili vilivyopo kwenye maeneo mbalimbali wilayani Rungwe

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Ikiwa kila ifikapo juni  16 Tanzania inaungana na mataifa mengine ya nchi za Afrika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kwa dhumuni la kumlinda mtoto na vitendo vya ukatili anavyo weza kutendewa kwenye jamii

wadau na wanafunzi walioshiriki kwenye maadhimisho ya mtoto wa afrika

Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Rungwe aliye wakilishwa na   Katibu tawala wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Ndg Ally Kiumwa amemwangiza mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Rungwe kufanya majadiliano upya ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili vinavyoendelea kuripotiwa licha ya kuwapo kwa mashirika yanayo tekeleza miradi ya kupinga ukatili dhidi ya watoto

katibu tawala ndg Ally kiumwa akizungumza siku ya maadhimisho ya mtoto wa afrika[picha na Lennox Mwamakula]

Kiumwa ametoa kauli hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika yaliyofanyika  kwenye viwanja vya shule ya msingi katumba II Iliyopo kata ya ibighi wilaya Rungwe ambapo amesema kuna haja ya jamii kuungana kupinga vitendo hivyo na kutoa taarifa kwa viongozi wa maeneo yetu wakiwemo wenyevit wa mitaa /vijiji na kwenye maadawati ya kutetea haki za mtoto

Mmoja ya wanafunzi akisoma risala mbele ya mgeni rasmi[ picha na lennox Mwamakula]

sauti ya kiumwa 1

Akisoma Risala mmoja ya wanafunzi wa shule ya msingi katumba II wanafunzi wamebainisha changamoto zinazowakabili kwaani wamesema lisha ya serikali kufanya jitihada mbalimbali ya kukabiliana  na vitendo vya ukatili, bado vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinaendelea  kama vile kubakwa,kurawitiwa ,mimba za utotoni na kukosa mirathi pindi wazazi wao wakifariki

sauti ya risala 1

Hata hivyo wanafunzi hao wameioma serikali kuwajengea miundombinu rafiki ya kufundishiwa ili kuwawezesha kupata elimu jumuishi na kuweka mazingira rafiki

sauti ya risala 2

Akijibu risala hiyo katibu tawala wa wilaya ya Rungwe Ally Kiumwa amewaomba wazazi kuto wafisha watoto wenye ulemavu kwani amesema hata wao wana haki ya kupata mahitaji yote ya msingi ikiwa ni pamoja na elimu hivyo jamii ijenge tamaduni ya kuwapeleka watoto waote shule ili waweze kupata haki zao za msingi

sauti ya kiumwa 2

Kwa upande wake afisa miradi kutoa shirika la Dsw Tanzania  amesema watandelea kushirikiana na serikali kukabiliana na kupinga vitendo vya ukatili na amewaomba wana Rungwe kutoa  ushirikiano kwa wadau waliopo kwenye maeneo yao

sauti ya afisa mradi 1

Ikumbukwe kuwa  chimbuko la maadhimisho ya mtoto wa afrika ni Azimio lililopitishwa na ulikuwa nai umoja wa  Nchi huru za kiafrika [OAU] Mwaka 1990 kwa lengo la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto nchini afrika kusini waliouwawa  tarehe 16 Juni,mwaka 1976 kutokana na ubaguzi wa rangi.