Chai FM

Polisi Rungwe kuja na mpango kabambe wa kutokomeza ukatili

13 May 2024, 6:08 pm

Kulia ni Mrakibu wa Polisi Janeth Masangano akipeana mkono na msaidizi wa kisheria wilaya ya Rungwe Ndg. Eddy Mwangalaba baada ya kukutana studio za Chai FM radio mapema leo. (Picha na Sabina Martin)

Jukumu la kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili ni la kila mtu kwa mujibu wa sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2019.

Na Sabina Martin – Rungwe

Kukua kwa utandawazi imetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazosababisha ongezeko la vitendo vya ukatili, huku waelimishaji katika mitandao ya kijamii wakihusishwa zaidi.

Akizungumza katika kipindi cha Amka na Chai mapema leo Mei 13, 2024 afisa ushirikishwaji wa jamii wilaya ya Rungwe Mrakibu wa polisi Janeth Masangano amesema wanawake kufanya majukumu ya waume zao katika familia ni sehemu ya ukatili kwa wanawake.

Aidha amesema kuwa wanawake wengi wanatumia mitandao ya kijamii kujifunza viu vingi na kufanyia kazi hisia za watu wengine hali inayosababisha migogoro kwa baadhi ya familia.

Sauti ya mrakibu wa polisi Janeth Masangano

Katika hatua nyingine Mrakibu wa Polisi Janeth ametoa rai kwa wazee wa mila kuzungumza na watoto wao, kuwaelimisha juu ya vitendo vya ukatili huku akisisitiza kwamba jeshi la polisi wataendelea kuelimisha zaidi watoto na walezi kuhusu malezi na ukatili.

Sauti ya mrakibu wa polisi Janeth

Sambamba na hilo jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia wilayani Rungwe limesema vitendo vya ukatili vinaendelea kushamiri kwenye jamii  kutokana na kutotoa  taarifa kwa viongozi waliopo maeneo yao licha ya elimu inayoendelea kutolewa.