Chai FM

Baada ya daraja kubomoka wananchi wakosa huduma Rungwe

4 April 2024, 6:45 pm

wananchi wakishuhudia daraja likisobwa na maji baada ya mvua kunyesha[picha na Lennox Mwamakula]

Jamii imeshauriwa kutolima kwenye vyanzo vya maji kwani kunapelekea madhara makubwa kwenye shughuli za kibinadamu.

Rungwe-Mbeya

Na lennox Mwamakula

Wananchi wilayani Rungwe wameiomba serikali kuwajengea daraja lililo bomoka katika mto Ibolelo hali iliyosababisha kukatika Kwa mawasilino baina ya  wakazi wa kata ya Ibighi na Bulyanga.

Daraja Hilo limebomoka kufuatia mvua zinazoendelelea kunyesha wilayani hapa na kusababisha baadhi ya barabara kutopitika na shughuli za kibinadamu kusimama kutokana na mito kujaa maji na madaraja kusombwa na maji.

Wananchi wametoa kilio hicho kutokana na daraja la ibolelo linalo unganisha kijiji Cha Lubiga na Bulyaga kukatika na wananchi kushindwa kusafirisha mazao Yao kama vile ndizi, maziwa pamoja na mahindi Toka mashambani.

.sauti za wananchi

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji Yona Mwalugaja amewashukuru wakazi wa Lubiga kwa kujitokeza kwani amesema baada ya wananchi kupata taarifa wakaamua kujenga daraja la dharula ili kuwezesha watoto waendao shule waweze kupita.

sauti ya mwenyekiti

Aidha naye mwakilishi wa diwani wa kata ya Bulyaga Bw………..amemuomba mwenyekiti wa eneo Hilo kufanya tathimini ya vitu vinavyo hitajika kama vile mbao na misumari  ili  vinunuliwe haraka kwajili ya kujenga daraja la muda la kuwezesha mizigo kuvushwa Kwa kutumia pikipiki

Wakala wa Barabara za mijini na vijijini wakipima ili kuweza kujenga daraja linalo unganisha kata ya Bulyaga na ibighi [picha na Lennox Mwamakula]

.sauti ya nwakilishi wa diwani

Kwa upande wao wakala wa Barabara za mjini na vijijini (TARURA)wilaya ya Rungwe wametaka wananchi wakata hizo mbili Bulyaga na Ibighi kuwa ujenzi wa daraja hilo utaanza mara moja kwani wamesema vipimo vyote vimechukuliwa hivyo ofisi inaenda kufanya tathimini ya gharama ya ujenzi wa daraja hilo.

sauti ya wakala wa Barabara za mjini na vijijini