Chai FM

Jamii iwe makini wizi mtandaoni

26 October 2021, 9:07 am

RUNGWE

Jeshi la polisi Wilayani Rungwe limewaomba wafanyabishara kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kukabiliana na watu wanao jihusisha na uwizi wa mtandaoni.

Jeshi hilo limetoa kauli hiyo kupitia Mkuu wa upelezi Wilaya ya Rungwe WILLIAM NYAMAKOMANGO alipokutana na wafanyabiashara kwenye ukumbi wa halmashauri wa john mwankenja kwenye kikao kilicho hitishwa na mkuu wa wilaya  cha kujadili changamoto wanazo kabiliana nazo wafanyabishara hao na kuzitafutia ufumbuzi wake.

NYAMAKOMANGO amesema kutokana na kuwepo na wimbi la uwizi kwanjia ya mtandao njia pekee ya kukabiliana na watu wanao jiusisha kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili kudhibiti vitendo hivyo.

Pia amewaomba wafanyabiashara hao kuwa na utaratibu wa kuajili walizi sehemu za kazi zao ili kuweka uwepesi kwa jeshi la polisi kupata taarifa kwa urahisi pindi matukio ya uwizi yanapo tokea.

Hata hivyo NYAMAKOMANGO amesama jeshi la polisi wilaya linawaomba wananchi kuwa na utaratibu wa kuanzisha ulinzi shirikishi kwa maeneno wanao ishi ili kuweza kutokomeza vitendo vya uwalifu vinavyo jitokeza kwenye jamii.