Chai FM

wakulima elfu 17 tayari wamesajiliwa Mbolea ya ruzuku

9 September 2022, 9:51 am

RUNGWE-MBEYA

NA:LETHISIA SHIMBI

Wakulima wilayani rungwe Mkoani mbeya wametakiwa  kufuata taratibu  wa kujisajili  kwenye mfumo Ili kuweza kupata Ruzuku za pembejeo.

Akizungumza na kituo Chai FM  afisa kilimo wilayani  hapa JUMA MZARA amesema katika halmashauri ya Rungwe wamesajiri wakulima elfu 17 kupitia mfumo na wamepata namba ya usajili.

Aidha ameendelea kwa kusema kuwa wakulima ambao hawajapata namba kutokana na changamoto za kimfumo wataenda kuwapatia namba pindi mfumbo utakapofanikiwa kukamilisha taarifa zao.

Pia MZARA amesema kuna mawakala kadhaa ambao waliomba  vibali vya kusambaza pembejeo  tayari washaanza kufanya kazi ya kugawa mbolea za Ruzuku kwa wakulima na kwa mfumo wa mwaka huu mkulima wa kijijini anatakiwa kwenda kununua mbolea ya ruzuku kwenye maduka ya pembejeo ya mawakala.