Chai FM

Wanawake wilayani wakomesha ukatili

9 December 2023, 5:07 pm

kufuatia na kuwepo kwa vitendo vya ukatili kwenye jamii wanawake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuripoti kwenye vyombo vya sheria.

RUNGWE-MBEYA

Na Lethicia Shimbi

Ikiwa bado ni Mwendelezo wa kampeni za kupinga ukatili wa kinjinsia Duniani  Wanawake Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wametakiwa kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia pindi tendewa majumbani kwao.

Hayo ameongea Lusajo Fred Kibonde Kaimu Mwenyekiti wa mtandao wa polisi wanawake Wilaya ya Rungwe wakati wa akikabidhi vifaa kwa wanawake waliojifungua katika hospitali ya wilaya Rungwe[ Makandana] amesema kuwa mwanamke yeyote atakaye fanyiwa kitendo cha ukatili wa kijinsia ni vyema akafika kwenye dawati la jinsia ili kutoa taarifa.

sauti ya kaimu mwenyekiti Lusajo kibonde

kaimu mwenyekiti wa mtandao wa polisi wanawake akikabidhi moja ya bidhaa kwenye hospitali ya wilaya[picha na lethicia shimbi]

Lusajo Kibonde amesema kuwa kupitia mtandao wa polisi wanawake wilaya ya Rungwe wameamua kufika hospitalini hapo kwa lengo la kutoa elimu na kukabidhi vifaa hivyo kama vile sabuni , sukari,pamoja na pampasi za watoto kwa mama aliyetoka kujifungua  kwani wanawake wamekuwa walengwa wakubwa wa kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.

sauti ya kaimu mwenyekiti

Naye Bupe Sucka kitengo cha Dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi Wilayani hapa amewaomba wanawake kuwa karibu na watoto wao ili waweze kubaini vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa na kuweza kutoa taarifa kwenye dawati la jinsia  .

sauti ya Bube sacka

Kwa upande wake Nesi wa Hospitali ya Wilaya  ameshukuru kitendo kilichofanywa na mtandao wa polisi mwanamke Wilaya ya Rungwe kwa kuwafikia wanawake na kuwapatia mahitaji hayo  na amewashauri wanawake wote kutokuwa na miyo ya kukata tama pindi wanapokutana na vitendi vya ukatili wa kijinsia

baadhi ya vitu vikikabidhiwa na wanawake wa dawati la mtandao la jeshi la polisi wilayani Rungwe[picha na lethicia shimbi]

sauti ya nurse wa hospitali ya wilaya

Sanjali na hayo baadhi ya wanawake waliyotembelewa na kupatiwa mahitaji hayo wametoa shukurani na kuwataka waendelee na moyo huo wa utoaji.

mmoja ya wanawake waliotembelewa hositalini hapo akikabidhiwa moja ya zawadi kwenye wodi la wazazi

sauti ya wanufaika

Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia huanza kila ifikapo novemba 25 na kufikia kilele decemba 10 ya kila mwaka ikiwa na lengo la kutokomeza vitendo vya ukatili kwa jamii huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “wekeza kuzuia ukatili wa kijinsia”.