Chai FM

Wananchi waitumie wiki ya sheria kupata msaada wa kisheria

26 January 2022, 8:50 am

RUNGWE-MBEYA

Kuelekea kilele cha wiki ya sheria nchini mahakama wilayani Rungwe imewataka wananchi kujitokeza katika maeneo ambayo zoezi la utoaji elimu litakuwa likifanyika .

Akizungumza na Radio Chai Kaimu Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Rungwe Bw.Augustine Lugome amesema  utaratibu huu  wa mahakama kuwa na wiki ya utoaji elimu unawapa fursa wananchi kufahamu kazi ya Mahakama na wale wanaohitaji msaada wa kisheria katika masuala mbalimbali wanapatiwa utatuzi bila malipo.

Aidha lugome amesisitiza kuwa utaratibu huu utaambatana na vibanda vya utoaji elimu katika maeneo ya wilaya ya Rungwe kuanzia tarehe 23 hadi tarehe 29 mwezi huu ambapo wananchi wapata elimu katika masuala ya kisheria.

Kaulimbiu ya Wiki ya Sheria kwa mwaka 2022 yanaeda na ujumbe usemao Zama za Mapinduzi ya 4 ya viwanda safari ya maboresho kuelekea Mahakama Mtandao.

Hata hivyo Kaimu Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Rungwe amewaalika wananchi kujitokeza kwenye kilele cha wiki ya sheria  tarehe 1 mwezi wa  pili  mwaka huu ambapo hafla za kilele zitafanyika katika viwanja vya Mahakama wilayani Rungwe.