Chai FM

Matumizi ya dawa kiholela chanzo cha magonjwa sugu

16 December 2022, 11:53 am

 

RUNGWE,

Imeelezwa kuwa matumizi ya dawa za binadamu bila kufuata ushauri wa daktari ni chanzo cha usugu wa magonjwa na hatimaye kupelekea kifo.

Hayo yamesemwa na mganga mkuu wa Wilaya ya Rungwe Dkt Diokles Ndaiza wakati akizungumza na Chai fm na kusema jamii imekuwa na mazoea ya matumizi ya dawa bila kuandikiwa na daktari hali inayoweza kuleta athari ya ugonjwa kutotibika.

Pia amesema ni vyema mgonjwa akaenda kituo cha kutolea huduma za afya kupata vipimo na kuandikiwa dawa inayotakiwa kulingana na maradhi husika ili kuepuka vifo visivyotarajiwa na usugu wa dawa.

Aidha Dkt Ndaiza  amewatahadhalisha  watu wanao fungua maduka ya dawa za binadamu  bila kufuata sheria Serikali itawachukulia hatua kali dhidi yao huku akisema wapo kwenye msako mkali wa maduka yenye vigezo vya kufanya biashara hiyo.

Hata hivyo akusita kutoa wito kwa wahudumu wa afya kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa na kutoa huduma bora pale wananchi wanapokwenda katika vituo vya afya.

Sambamba na hayo  nao wauzaji wa maduka ya dawa za binadamu wamesema kuna changamoto ya elimu kwa jamii katika matumizi ya dawa kulingana na maradhi.