Chai FM

Rungwe yazindua programu jumuishi kupuguza tatizo la afya ya akili

30 October 2023, 9:33 am

Matatizo mengi ya afya ya akili ni matokeo ya kutozingatia malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto katika hatua zake za ukuaji kwa kipindi cha kuanzia mwaka 0-8.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia magunzo ya utekelezaji wa program jumuishi ya kitaifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto( picha na Noah Kibona)

Na Sabina Martin – Rungwe

 Utekelezaji madhubuti wa programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto imetajwa kuwa chanzo cha kupunguza tatizo la afya ya akili kwa kizazi kijacho.

Akizindua programu jumuishi ya taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ngazi ya wilaya mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambaye pia ni mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii halmashauri ya Rungwe Bw. Godson Harry amesema kuwa halmashauri inatarajia kutenga bajeti kwaajili ya utekelezaji wa programu hii.

Aidha amesema kuwa utekelezaji wa programu hii unategemea ushirikiano zaidi kutoka kwa wadau huku akiongeza kwamba endapo mtoto akikosa malezi bora ni chanzo cha tatizo la akili.

Sauti ya mgeni Rasmi

Yona Mwakatobe ni afisa uchechemuzi mwandamizi kutoka shirika lisilo la kiserikali la SHALOM amesema kuwa mtoto asipokuzwa vizuri anapoteza kujiamini na wakati mwingine huwa na kiwango kidogo cha uelewa.

Sauti ya afisa mchechemuzi

Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi huo CDO kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Bi. Elukaga Mwalukasa ameeleza kwamba Programu hiyo inazingatia fursa ya ujifunzani wa awali, afya bora, malezi shirikishi na ulinzi na usalama.

Sauti ya CDO Mbeya

Baadhi ya washiriki waliohudhuria uzinduzi huo walikua na haya ya kusema

Sauti za washiriki

Programu jumuishi ya taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto inatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano (2021/22-2025/26) wenye lengo la kutatua changamoto za ukuaji na maendeleo ya watoto wenye umri wa miaka 0-8.