Chai FM

Jamii itoe taarifa kuhusu vitendo vya ukatili

9 September 2022, 9:57 am

RUNGWE-MBEYA.

NA:LETHISIA SHIMBI

Baadhi ya Wanawake Wilayani Rungwe mkoani Mbeya  wameeleza namna wanavyoshiriki kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo.

Wakizungumza na chai fm BAHATI SIMON na MAIDASI NDAMU wamesema endapo vitendo vya kikatili vikajitokeza kwenye jamii wapo tayari kutoa ushirikiano na kumsaidia mhusika kufika eneo husika kupata msaada wa kisheria.

Kwa upande wao wananchi  wilayani Rungwe  wamesema vitendo vya kikatili vimekithiri kwenye jamii hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kutoa taarifa za vitendo vya kikatili bila kusita kuanzia ngazi ya kijiji hadi Wilaya ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo.

Naye  Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto na makundi maalum  DKT.DOROTHY GWAJIMA amesema Serikali inaendelea kupambana na vitendo vya ukatili  na  kuwataka wananchi  kuendelea kufichua vitendo hivyo.