Chai FM

4326 kufanya mtihani wa kidato Cha nne Rungwe

10 November 2021, 5:57 am

Jumla ya wanafunzi 4,326 wilayani Rungwe mkoani Mbeya wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne unaotarajiwa kuanza tarehe 15.11.2021 kote nchini.

Afisa elimu sekondari wilaya ya Rungwe Mwl. Yona Mwaisaka

Kwa mujibu wa Afisa elimu sekondari wilayani Rungwe Mwl. Yona Mwaisaka amesema kati ya watahiniwa hao 231 ni wakujitegemea na 4095 ni watahiniwa wa shule huku vituo vya kufanyia mitihani vikitarajiwa kuwa 38.

Kuhusu udanganyigu katika mitihani afisa elimu huyo amesema kwamba kamati ya mitihani ya wilaya imejiandaa vyema hivyo hategemei kitu kama hicho katika wilaya ya Rungwe.

Katika hatua nyingine amehimiza wazazi kushirikiana wote kwa pamoja ili watoto wapate chakula shuleni ili kuongeza zaidi kiwango cha ufaulu, huku akitoa rai kwa viongozi wa dini kuendelea kuwaombea wanafunzi wafanya mitihani yao vyema kwa kipindi chote kama ilivyoainishwa katika ratiba.

Hata hivyo ametoa rai kwa wanafunzi kuendelea kujisomea kipindi hiki cha maandalizi kuelekea mitihani yao ya mwisho, huku akisisitiza kuzingatia sheria za mitihani kipindi chote cha mitihani.