Chai FM

Vijana wachangamkie mikopo ya halmashauri

16 February 2022, 10:03 am

RUNGWE-MBEYA.

NA:JUDITH MWAKIBIBI

Wananchi wilayani Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa  kujiunga na vikundi mbalimbali ilikuweza kunufaika na mikopo inayotolewa na Halmashauri ikiwa ni vikundi vya watu wenye ulemavu ,wanawake na vijana.

Akizungumza na redio Chai FM ofisini kwake Mratibu Wa Dawati  La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi   Teddy Siame amesema kuwa ili mwananchi aweze kupatiwa mkopo kuna taratibu ambazo  anatakiwa kuzifuata na amesema ili kikundi kiweze kukopeshwa kikundi kiwe kimekaa miezi sita  au mwaka mmoja hiyo itasaidia wanakikundi kujuana zaidi.

Ameongeza kuwa vikundi hivyo kabla ya kupewa mkopo wamekuwa na utaratibu wa kutembelea vikundi hivyo na kuwapatia elimu jinsi ya kuzirudisha fedha hizo baada ya kukopa na kuwez kujiridhisha kama miradi waliombea mkopo imekuwa ikiendelea.

Kwa upande wa kikundi cha bam investment kilichopo buliyaga ambacho ni moja ya wanufahika mikopo hiyo mwenyekiti wa kikundi hicho Baraka  Mwampulule amesema kuwa kuna mafanikio makubwa ambayo wamepata kutoka na mkopo huo ikiwa ni pamoja kununua mashine mbalimbali kwajili ya utengenezaji wa viatu.

Nao baadhi ya vijana ambao hawajanufaika na mikopo hiyo wamesema wanashidwa kujiunga katika vikundi kutokana na vijana kukosa uwaminifu jambo linalopelea kurudi nyuma kimaendeleo.