Chai FM

Wivu wawanyima uhuru watumishi

13 October 2021, 8:56 am

RUNGWE-MBEYA

Wivu wa maendeleo imetajwa kuwa moja kati ya sababu zinazopelekea waajiri wengi wa wafanyakazi wa majumbani kutowaruhusu wafanyakazi wao kuendesha miradi yao.

Mwadishi wetu akifanya mahojiano na wananchi

Wakizungumza na waandishi wetu baadhi ya wananchi wilayani hapa wamesema kwamba baadhi ya waajiri wanaogopa kuzidiwa kipato na wafanyakazi wao hivyo hawatoi uhuru kwa waajiri wao kuendesha miradi yao.

Tamali ambaye si jina lake halisi amesema kwamba waajiri wengi hawawapi uhuru wa kufanya shughuli zao binafsi kwaajili ya kujipatia kipato.

Hadija Ahmed ni mshauri wa ujasiliamali wilayani hapa amesema kwamba kumpa uhuru mfanyakazi ajidhughulishe na shughuli zake binafsi itasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuwa tegemezi.