Chai FM

Kilimo cha strawberry chachu kwa wakullima wilayani Rungwe

13 September 2023, 10:45 am

Muonekano wa mmea wa strawberry ukiwa shambani kabla ya kutoa matunda(picha na Lennox Mwamakula

Kutokana na wilaya ya Rungwe kuwa na kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula, biashara, matunda na mbogamboga rai imetolewa kulima pia zao la Strawberry kutokana na zao hilo kustawi wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Na Evodier Ngeng’ena – Rungwe
Wakulima wilayani Rungwe wametakiwa kuwa na huakika wa masoko kwa bidhaa wanazolima ili kuzalisha kulingana na mahitaji ya soko.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa KIBOWAVI [Kilimo Bora Cha Mboga Na Matunda Kwa Vijana] Daniel Kalimbiya alipotembelea shamba la strawberry linalomilikiwa na mkulima Jotham Marakibungu
katika kijiji cha Syukula kata ya Kyimo wilayani Rungwe.

Sauti ya mkurugenzi KIBOWAVI

Kwa upande wake Jotham Marakibungu ambaye ni mkulima wa strawberry ameishukuru Kibowav kwa kumpatia elimu juu ya zao al strawberry na kuwasihi watu wengine kulima zao hilo kwani lina tija na huvunwa mara tatu kwa wiki.

Sauti ya mkulima wa zao hilo

Nao baadhi ya wakulima waliofika katika shamba hilo wameeleza kuhamasika kuanzisha kilimo hicho cha strawberry kama ilivyo kwa Jotham Marakibungu.

Sauti za wakulima

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Syukula Akim Mwakipesile amewakaribisha watu wote wanaotaka kujifunza kulima strawberry kwenda kujifunza katika kijiji cha Syukula akta ya Kyimo.

Sauti ya mwenyekiti