Chai FM

Jamii yatakiwa kutunza mazingira Rungwe

26 April 2024, 2:09 pm

katibu tawala wa wilaya ya Rungwe Ally Kiumwa akisoma taarifa mbele ya mkuu wa wilaya kwenye siku ya maadhimisho ya miaka 60 ya muungano [picha na Lennox Mwamakula]

wananchi wametakiwa kuendelea kudumisha amani iliyopo kwa kulinda muungano wa tanzania

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Serikali imewataka wananchi kuachana na matumizi ya nishati ambayo si safi kama matumizi ya mkaa yanayo sababisha uwalibifu wa mazingira kwa kukata miti ovyo

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Hanniu akiwahutubia wananchi siku ya maadhimisho ya Muungano [picha na Lennox Mwamakula]

 Kauli imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh, Jaffar Hanniu leo April 26 mwaka 2024 katika sherehe za kumbukizi ya kuutimiza miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuundwa kwa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania

stendi ya ,abasi tukuyu wananchi wakiwa kwenye sherehe za muungano

sauti ya mkuu wa wilaya ya Rungwe

Akisoma taarifa katibu tawala wa halmashauriya ya Rungwe Ally kiumwa amesema katika maadalizi ya kuelekea kilele cha maadhimisho hayo halmasau ilifanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na ufanyaji wa usafi kwenye taasisi za umma na wananchi walishiriki kikamilifu kufanya usafi kwenye makazi yao

Pia Kiumwa amesema katika kuelekea maadhimicho hayo jumla ya miti imepandwa katika maeneo mbalimbali pamoja na kutoa elimu kwa jamii umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji na kujikita katika upandaji wa miti kwenye maeneo wanayoishi ili kukabiriana na mabadiliko ya Tabia ya nchi

sauti ya katibu tawala

katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Rungwe Abdallah Mpokwa [picha na Lennox Mwamakula]

Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi wila Rungwe Abdallah Mpokwa ametumia nafasi hiyo kwa kuwakumbusha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ili kuweza kuchagua viongozi wanao wataka taifa linapo elekekea kwe uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu  mwaka 2025

…………KATIBU