Chai FM

Machinga kutii agizo la serikali

25 October 2021, 9:21 am

RUNGWE

Wafanya biashara wadogo (machiga) soko la Tukuyu, wamesema wameanza kutekeleza agizo la Halmashauri la kuhama katika maeneo yasiyo rasmi wanayo fanyia biashara zao na badala yake wahamie katika maeneo waliyo pangiwa na halmashauri.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na radio chai fm,Ambapo wamesema wamelipokea agizo hilo la halmashauri la kuhama ndani ya siku saba katika maeneo yao ya awali licha ya kwamba itawapa wakati mgumu kuyazoea maeneo mapya waliyo pangiwa.

Aidha wameongeza kwa kuiomba Halmashauri ya wilaya Rungwe igawe maeneo ya biashara zao kulingana na biashara zao kwani awali kulikuwepo na mgao wa maeneo usio fuata uhalisia wa biashara zao.

Mwenyekiti wa machinga Jobuu Mwambelo, amesema kufuatia kutokea kwa mabadiliko hayo ya machinga kuhamishwa katika maeneo yao kumekuwa na mapokeo tofauti kutokana na baadhi ya machinga hao kuto kuafiki kuhamishwa katika maeneo yao hayo ya awali.

Sambamba na hayo Mwambelo amemaliza kwa kuwaomba machinga wote wilayani Rungwe waiheshimu kazi yao kama ajira na ofisi zao ambazo zitawasaidia wao kujipatia kipato chao na serikali kwa ujumla.