Chai FM

Wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwenye vyombo vya maamuzi Rungwe

1 February 2024, 2:47 pm

katika kuadhimisha siku ya sheria jamii pamoja na wadau mbalimbali wameaswa kuwa na utaratibu wa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya maamuzi kama mahakama.

Aakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya akizungumza na wadau washeria[picha na Lennox Mwamakula]

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Wananchi wameshauriwa kupeleka mashauri Mbalimbali wanayo kabiliana nayo kwenye vyombo vya maamuzi ili yaweze kutatuliwa kwa kufuata sheria.

Kauli hiyo imetolewa na Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Rungwe Ramla Shehagila kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya sheria ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya mahakama ya wilaya ya Rungwe amesema kutokana na kwamba sheria inazitaka mahakama kutenda haki bila ubakuzi hiyo kila raia inampasa kutoa ushirikiano ili kuiwezesha mahakama ya Tanzania kutimiza jukumu la utoaji haki

sauti ya mgeni rasm

Awali akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi wakili wa serikali kutoka ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Rungwe Rosmery Ngenyi amesema dhamira ya ofisi ya mwendasha Mashtaka ni kuiwezesha serikali inayo andaa miswada na bunge linalo tunga sheria kutekeleza majukumu ili kuwezesha taifa kuwa na sheria nzuri.

Mkuu wa wilaya Rungwe Jaffar Hanniu

sauti ya DPP

Hata hivyo amewakumbusha viongozi wa serikali mbalimbali kuzingatia miongozo inayotolewa ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi kama vile kuwepo kwa madai ya kuwekwa Maabusu kinyume na Sheria,kukamatwa bila kufuata utaratibu na kupewa Adhabu mbalimbali kinyume na sheria

Mwendesha mashitaka ya wilaya ya Rungwe akisoma taarifa mbele ya mgeni Rasmi[Picha na Lennox Mwamakula]

Sauti ya DPP 2

Kwa upande wa chama cha wanasheria nchini TLS wamesema kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo Mawakili wanakutana nazo wawapo mahakamani kama vile uchelewashwaji wa kesi,makama nyingi za mwanzo kutokuwa na chumba maalum kwajili ya mawakili na kuwepo na vishoka wengi hivyo wameiomba Mahakama kuzifanyia kazi changamoto hizo.

wadau walioshiriki kwenye hafla ya siku ya sheria

sauti ya TLS

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Hanniu amewaomba wanachi wa wilaya Rungwe kutokana na kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi, amewataka wananchi kumaliza migogoro hiyo ngazi ya jamii ili kuondoa mlundikano wa mashauri Mahakamani.

Sauti ya kuu wa wilaya