Chai FM

Millioni 201 zajenga kituo cha afya Kinyala

19 January 2024, 10:47 am

Na Mwandishi wetu

Katika kuhakikisha sera ya afya ya kuwa na kituo cha afya kila kata halmashauri ya wilaya ya Rungwe imetekeleza kwa vitendo sera hiyo wa kujenga vituo vya afya katika kata mbalimbali ndani ya halmashauri yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Bw. Noah Kibona imeeleza kwamba zaidi ya shilingi million 201 zimetumika katika ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya kinyala.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba Fedha hizo zimetolewa na Halmashauri ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhakikisha kila kata inajengewa kituo cha afya.

Vituo vingine vinavyoendelea kujengwa  kwa kutumia mapato ya ndani ni vile vya kata za Masebe na MalindoHuku vituo vingine vilivyopokea fedha kutoka Serikali kuu na ujenzi unaendelea  ni vile vya kata za Kiwira na Masoko.

Hata hivyo Wakazi wa kata ya Swaya pia wanaendelea na ujenzi ambapo serikali imepeleka bati kwa ajili ya upauaji kupitia mfuko wa jimbo.

Vituo vilivyo kamilika na vinatoa huduma ni pamoja na Mpuguso, Isongole, Kyimo, Iponjola ,Kalebela, Ikuti, Masukulu na Ndanto.