Chai FM

Jamii kuepuka majanga ya moto Rungwe

28 March 2024, 6:54 pm

ili kuhakikisha majanga ya moto yanaepukika wananchi wanatakiwa kutoa taarifa juu ya majanga ya moto.

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Jeshi la polisi kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto na uokoaji wilayani Rungwe mkoani Mbeya limewataka wananchi wa mtaa wa Igamba kata ya Bulyaga kuwa wavumilivu na kusubiri upelelezi kufuatia tukio la Nyumba kuwaka moto na kuteketeza vitu mbalimbali.

polisi akitoa elimu kwa wananchi juu ya utoaji taarifa pindi majanga ya moto yanapotokea

Kauli hiyo imetolewa na mkaguzi msaidizi Salim Mgoo kutoka jeshi la polisi alipokuwa akizungumza na wananchi wa mtaa huo  baada ya kufanikiwa kuzima moto huku akiwataka wananchi wa mtaa huo kuwa watulivu mpaka pale upelelezi utakapokamilika ili kujua chanzo halisi kilichosababisha moto huo.

jeshi la zimamoto na uokoaji wakizima moto nyumba ilikuwa ikitetea kwa moto

sauti ya jeshi la polisi 1

Pamoja na hayo Mgoo amewaasa wananchi kuwa wepesi wa kupiga simu moja kwa moja zimamoto pale wanapopata ajali ya moto na majanga mengine katika maeneo yao ili waweze kufika kwa wakati na kutekeleza majukumu yao.

baadhi ya vitu vilivyo teketea ndani ya nyumba hiyo

sauti ya jeshi la polisi 2

Mmoja kati ya majirani wa eneo hilo amesema kuwa aliona moshi ukifuka kwenye moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo ndipo alipochukua jukumu la kuita majirani.

Amesema kuwa juhudi za awali zilianza kutolewa na wananchi wa mtaa huo ni kumwaga maji kwenye eneo lililozingirwa na moto na baadae wakafika zimamoto nakuzima moto huo wakishirikiana na wananchi.

sauti ya shuhuda