Chai FM

Ruzuku kwa wakulima wa maparachichi itasaidia uzalishaji wa tija.

23 February 2022, 5:21 am

RUNGWE-MBEYA

Mkuu wa walaya ya Rungwe Mkoani Mbeya Dkt VICENT ANNEY ameuomba uongozi wa  chama cha ushirika UWAMARU [AMCOS] kuwa na utaratibu wa kutoa ruzuku kwa wakulima wa maparachichi ili kuweza kuzalisha kwa tija.

Ametoa kauli hiyo kwenye kikao cha makabidhiano ya vifaa ya kuvunia parachichi kwenye ofisi za UWAMARU zilizopo kijiji cha Ilenge kata ya Kyimo na vifaa hivyo vimetolewa na HELVETAS.KIBOWAVI.

Exif_JPEG_420

Akisoma risala afisa ushirika wa AMCOS Ndg COSMAS BENARD amesema wanaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ili kuweza kutatua changamoto wanazokabiliana nazo kwenye zao la parachichi.

Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Mkuu wa wilaya ya Rungwe Dkt Vicent Anney amesema ili ushirika uweze kuendelea wakulima waweze kushirikishwa ili kuweza kuongeza uzalishaji zaidi wa zao hilo na kutaka kuwatafuta wanunuzi kutoka sehemu mbalimbali kwakufuta utaratibu ulio wekwa na Serikali.

Naye mkurugenzi wa program ya KIBOWAVI nyanda za juu kusini Ndg DANIEL KALIMBIYA ameeleza lengo la kikao hicho kuwa ni kukabidhi vifaa vya kuvunia na kuhifadhia zao la parachichi kutokana na mkulima kutokuwa na elimu ya namna ya uvunaji na zao hilo kukosa soko kutokana na uvunaji holela.

Nao wakulima walio hudhuria hafla hiyo wameshukuru uongozi wa UWAMARU kwa kuwatafutia wadau waliowapatia vifaa hivyo kwani wanakwenda kuondokana na changamoto wakati wa uvunaji na uwifadhi wa parachichi