Chai FM

Wazazi, walezi watajwa chanzo cha mimba za utotoni

7 December 2023, 4:54 pm

Malezi yasiyozingatia misingi bora pamoja na ukosefu wa elimu ya uzazi imetajwa kuwa chanzo cha mimba za utotoni wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Na Sabina Martin

Mimba katika umri mdogo imetajwa kuwa ni miongoni mwa ukatili uliokithiri katika jamii ya wananchi wa Rungwe mkoani Mbeya huku chanzo kikitajwa kuwa ni malezi yasiyozingatia misingi bora pamoja na ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi.

Wakizungumza katika kipindi cha Amka na chai mapema leo Disemba 12.2023 Afisa ustawi wa jamii mkoa wa Mbeya Bi. Aika Temu na Afande Bupe Sucka kutoka Dawati la jinsia kituo cha polisi Tukuyu wamesema kuwa watoto wengi wanaopata mimba katika umri mdogo ni matokeo ya ukatili huku malezi duni yakihusishwa.

Wadau wakiwa studio za chaifm Radio wakitoa elimu ndani ya siku kumi na sita ya kupinga ukatili

sauti ya Afande na Afisa ustawi

Bi. Mwanane Madebo kutoka shirika lisilokuwa la kiserikali la Care International kupitia mradi wa Her Money Her Life amesema Kutokana na ukosefu wa elimu kwa jamii juu ya vitendo vya ukatili shirika hilo limewajengea uwezo wanawake kujitegemea ikiwa ni pamoja na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii.

sauti ya Bi,Mwanane

Thobias Burton na Asha Samson ni baadhi ya wananchi waliopatiwa elimu na shirika la care International wamesema kwamba kabla ya kuelimishwa kuhusu suala la ukatili waliishi kwa mazoea ukilinganisha na hivi sasa.

sauti za wananchi