Chai FM

Wachungaji 17 wabarikiwa KKKT dayosisi ya Konde

17 January 2024, 11:07 am

Na mwandishi wetu

Askofu Geophrey Mwakihaba wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Konde amewabariki Wataradhia kumi na saba kuwa Wachungaji baada ya kuhitimu masomo ya Theolojia hivyo kuendelea kuongeza Watumishi ndani ya Kanisa ibada iliyofanyika usharika wa Tukuyu Mjini.

Kabla ya kuwabariki Wachungaji Askofu Mwakihaba amewataka Wachungaji kufundisha kwa usahihi neno la Mungu na kuisimamia sakramenti, huku akiwataka kuwa faraja kwa waumini kwani Mungu haangalii uzoefu bali anaangalia wito.

Mhubiri katika ibada hiyo Mchungaji Abel Mwaipaja kutoka Usharika wa Ngamanga Kyela Jimbo la Kusini amewataka waumini kumuomba Mungu na kuwalea watoto kwenye njia ya wokovu na baraka za Mungu huwa na ushindi.

 Awali Msaidizi wa Askofu Dayosisi ya Konde Mchungaji Dkt Meshack Njinga amewashauri waimbaji kuacha kutumia flush au CD katika uimbaji badala yake watumie vyombo au sauti zao kwani kutumia vitu hivyo katika ibada ni maigizo haimpi Mungu utukufu.

Nao baadhi ya Wachungaji Bujo Kajinga, Solomon Mwakisyanju,Annastazia Panja na Osward Sanga waliobarikiwa mbali ya kumshukuru Mungu kuwafikisha hatua hiyo wamesema wako tayari kumtumikia mahali popote watakapopangiwa na Kanisa.

Naye Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Konde Wakili Benjamin Mbembela amewataka waumini kuungana kuimarisha miradi yake zikiwemo shule na hospitali ili kanisa liondokane na michango ya mara kwa mara.

Kuingizwa kazini na kupatiwa mbaraka kwa wachungaji hao kutaondoa upungufu wa wachungaji ambao wamestaafu na baadhi walihamia madhehebu mengine. Ifahamile kuwa Wachungaji waliobarikiwa leowametoka katika vyuo vinavyotambulika na Kanisa