Chai FM

Ushirikishwaji wa Wananchi wazaa matunda Rungwe

7 March 2024, 2:43 pm

Na Mwandishi wetu

Muonekano wa mabweni na wanafunzi katika shule ya sekondari Isongole(picha na Yona Kibona)

Elimu ya utambuzi inayotolewa na serikali kwa wananchi imeendelea kuboresha miundombinu mbalimbali kama vile ya elimu.

Wakazi wa kata ya Isongole wilayani Rungwe mkoani Mbeya wamejenga bweni la wavulana katika shule ya sekondari Isongole ikiwa ni hatua ya kuboresha  kiwango cha ufaulu pamoja na kuwaepusha na vitendo hatarishi katika maeneo yao

Hatua ya kujenga mabweni imekuja baada ya wananchi hao kujionea watoto wao wakitembea umbali mrefu kitendo amacho baadhi ya wanafunzi wanao toka vijiji vya mbali kukosa baadhi ya vipindi.

Baadhi ya wazazi walizungumza na mwandishi wetu wamevitaja vijiji vinavyo patikana ndani ya kata hiyo kuwa ni pamoja na Ngumbulu, Isyonje na Ndwati.

Katika hatua nyingine wazazi hao wamesema kuwepo kwa mabweni shuleni hapo kutasaidia watoto wao wanaosoma katika shule hiyo kutojiingiza katika makundi mabaya kwani muda mwingi watautumia shuleni.