Chai FM

Taasisi ya Tulia Trust yadhamiria kuondoa umasikini kwenye jamii

12 December 2023, 12:59 pm

kutokana na kuto kuwepo kwa usawa ndani ya jamii taasisi ya Tulia Trust imeendelea na kampeni yake ya kukimbiza Bendera ikiwa imebeba ujumbe wa upendo, usawa na uwajibikaji wa kuwatembelea wenye mahitaji maalumu wilayani Rungwe.

Kiongozi wa mbio za bendera Bw. Joshua Mwakanolo akipeperusha bendera ya upendo katika kijiji cha Ilolo kata ya Kiwira wilayani Rungwe

RUNGWE..MBEYA

Na lennox Mwamakula

Taasisi ya Tulia Trust imemkabidhi kiti mwendo Ester Seme mkazi wa kijiji cha ilolo kata ya kiwira wilayani Rungwe mkoani Mbeya  kwaajili ya kumsaidia kufika maeneo mbalimbali.

Akikabidhi kiti hicho Joshua Mwakanolo Afisa Habari wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo kwaniaba ya mkurugenzi wa Taasisi hiyo Tulia Akson ambaye ni spika wa bunge la jamhuri ya muungano pia Rais wa mabunge Duniani amesema jamii inapaswa kusaidiana.

Sauti ya afisa habari Joshua Mwakanolo 1

Aidha Joshua amelishukuru Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini kwa kuamua kumsomesha kijana mwenye ulemavu.

Sauti ya afisa habari Mwakanolo 2

Seth Bukuku ni Mwenyekiti wa kijiji cha ilolo ameishukuru taasisi hiyo kwakuwaona wenye mahitaji waliomo ndani ya kijiji hicho.

Sauti ya mwenyekiti bw. Seth Bukuku

Naye Gwamaka Jongo Afisa Habari wa Kanisa la Moravian Jimbo ametoa neno juu ya taasisi ya hiyo namna inayo wajali jamii kwani kwani amesema bila kuwa na jamii yenye nguvu taifa haliwezi kusonga mbele.

Sauti ya Jongo

Akipokea kiti mwendo Jestina Seme Bibi ya mtoto amemshukuru ameishukuru taasisi ya Tulia kwa msaada walioutoa kwa familia hiyo.

Sauti ya Jestina Seme

Taasisi ya Tulia Trust imekuwa ikitoa misaada kwa wahitaji nchini hivyo kuwasaidia kuwaondolea kadhia mbalimbali .