Chai FM

Madiwani Rungwe waonywa kuingilia majukumu ya watendaji

1 November 2023, 7:40 pm

Mkurugenzi wa halmashauri ya Busokelo wa pili kutoka kulia akijiandaa kusoma majina ya waliopata tuzo.

Kutokana na baadhi ya madiwani kuingilia majukumu ya watendaji wa vijiji, imeelezwa imekuwa sababu ya kutofanya majukumu yao ipasavyo.

Na Evodia Ngeng’ena : Rungwe- Mbeya

Haniu amezungumza hayo kwenye baraza la madiwani la robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2023/2024 kwenye halmashauri ya busokelo wilayani Rungwe mkoani Mbeya ambapo amewataka madiwani kuacha mara moja tabia hiyo inayoweza kuleta migogoro baina yao na watendaji wa kata na vijiji kwenye maeneo yao.

sauti ya mkuu wa wilaya 1

Aidha hanniu amewataka madiwani kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali kwa kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inyotekelezwa kwenye maeneo yao.

sauti ya mkuu wa wilaya 2

Meckson Mwakipunga ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM amewaagiza maafisa watendaji vijiji kuondoa kero ndogo ndogo zinazojitokeza kwenye maeneo yao ikiwemo changamoto ya utozaji faini holela na kuwakumbusha kusoma mapato na matumizi kwa wakati kwa mujibu wa sheria.

Mkuu wa wilaya akikabidhi vyeti kwa watumishi[picha na peter Tungu]

sauti ya mwenyekiti wa chama

pamoja na mambo mengine halmashauri ya busokelo imetoa tuzo kwa watumishi mbalimbali wa hamlashauri hiyo waliofanya vizuri kwenye idara zao ikiwemo ukusanyaji wa mapato, ambapo kwa wale waliofanya vizuri walipata fedha pamoja na vyeti vya pongezi huku afisa mtendaji wa kijiji na kata ya Isange wakipata vinyago kutokana na kufanya vibaya kwenye ukusanyaji mapato.

sauti za watumishi