Chai FM

Makusanyo hafifu ya mapato yawafukuzisha kazi watendaji

9 November 2021, 6:09 pm

KYELA-MBEYA

Halmashauri ya wilaya ya kyela mkoani Mbeya imeagizwa kuwafuta kazi watendaji wa kata  ambao kata zao zimekuwa za mwisho kwenye zoezi la ukusanyaji wa mapato.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera mbele ya baraza la madiwani wa halmashauri ya kyela alipopata nafasi ya kutoa  vyeti  kwa watendaji wa  kata  pamoja na mawakala wa ukusanyaji wa mapato ambao wanatekeleza vizuri zoezi la ukusanyaji wa mapato.

Homera amesema kuwa serikali haiwezi kuwavumilia watendaji ambao hawako tayari kuwajibika ipasavyo kwenye majukumu yao, na hatimaye kupelekea kata zao kuwa za mwisho kila mara.

Aidha ametoa wito kwa halmashauri zote mkoani mbeya kuiga mfano wa halmasahuri ya wilaya ya kyela kutoa zawadi kwa watendaji na wakusanya mapato wote wafanyao vizuri pasina kusahau kuwaondoa wale wafanyao vibaya ili kuhakikisha zoezi la ukusanyaji wa mapato linaenda vizuri kwa maslahi mapana ya wananchi.

Miongoni mwa kata ambazo zoezi la ukusanyaji limefanikiwa kwa kiwango kikubwa ni pamoja na kata ya Kajunjumele,Ipinda na Ikimba huku zikiongozwa na kata ya Njisi ambayo ukusanyaji wake wa mapato ulifikia  asilimia 138.