Chai FM

Jamii iwapeleke watoto wapate chanjo ya polio

10 September 2022, 7:47 am

RUNGWE-MBEYA

NA:WANDE BUSHU

Mratibu Wa Chanjo Katika Halmashauri Ya  Wilaya Rungwe Mkoani   Mbeya Ezekiel Mvile Amewaomba Wazazi Kuwapeleka Watoto Wao Katika Vituo Vya Afya  Waweze Kukamilisha  Dozi Ya Polio ili Iweze Kuwakinga Na Ugonjwa Huo.

Ameyasema Hayo Wakati Akizungumza Na Chai Fm Huku Akieleza Kuwa Kundi Kubwa  Linaloathirika Na Ugonjwa huo  Ni Watoto Walio Chini Ya Umri Wa Miaka Sifuri  Hadi Miaka Kumi Na Tano.

Aidha Mvile Ameongeza Kuwa Kwa Mujibu Wa Utaratibu Wa Serikali Watoto Chini Ya Umri Wa Miaka Mitano Ndio Wanatakiwa Kupata Chanjo Ya Polio Na Endapo Mtoto Amepata Chanjo Awali Na amevuka Umri Wa Miaka Mitano Anatakiwa Amalizie Dozi Hizo Kwani Hazina Madhara

Pia Mvile Amehitimisha Kwa Kusema Kuwa Mtoto Ili Awe Amekingwa Kikamilifu Na Ugonjwa Huo Anatakiwa Apate Dozi Nne  Za Chanjo Ya Polio.

Kwa Upande Wao Wananchi Wa Wilaya Ya Rungwe Wamesema Hawana Uelewa Wowote Kuhusiana Na Ugonjwa Huo Hivyo Wamewaomba Wataalamu wa afya Kuwapatia Elimu Juu Ya Ugonjwa Huo.