Chai FM

Mikopo ya halmashauri mkombozi kwa vijana Rungwe

5 May 2025, 4:24 pm

serikali imeombwa kupunguza masharti ya kupata mikopo kwa vikundu vya vijana.wanawake na watu wenye ulemavu

RUNGWE-MBEYA

Na Neema Nyirenda

Baada ya serikali kufungua dirisha la mikopo awamu ya kwanza ya asilimia kumi ya halmashauri kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu baadhi ya wana  vikundi wilayani Rungwe vimelalamikia masharti yaliyowekwa  namna  ya kupata mikopo hiyo

Wakiongea kwa nyakati tofauti na ChaiFM  baadhi ya vijana wamesema wameshindwa kupata mkopo kutokana na vigezo vilivyo wekwa  na halmashaurii kwani inaonyesha serikali ilikuwa na malengo mazuri kwa wananchi wake ila kuna daadhi ya watumishi wana kwamisha watu kupata mikopo hiyo

Kaimu Afisa maendeleo ya Jamii wilaya ya Rungwe Israel Alimwene akiongea na wanahabari ofisini kwake

sauti ya kijana

Aidha naye Bi, Jestina Chaula ni mkazi wa Rungwe ameshangazwa na vitendo vinavyofanya na watumishi kuwazungusha bila mafanikio yoyote kwa madai kuwa hawezi kupatiwa mkopo kutokana na umri wake

sauti ya jestina chaula

Israel Alimwene nia afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Rungwe amebainisha sifa za kikundi  amesema kikundi ni lazima kiwe na katiba na kisajiliwe na hata shughuli zinazofanyika ndani ya kikundi husika zijulikane

sauti ya kaimu afisa maendeleo 1

Hata hivyo Alimwene  amesema serikali imeboresha mikopo kwakutambua changamoto wanazo pitia watu wenye ulemavu nchini kwa kuwapatia mkopo wa mtu mmojammoja na si kwa vikundi .

sauti ya kaimu afisa maendeleo ya jamii 2