Chai FM
Chai FM
5 May 2025, 5:27 pm

ili kujiletea maendeleo wananchi wanatakiwa kushiriki kwenye mikutano kawenye maeneo yao
RUNGWE-MBEYA
Na Derick Gwakisa
Wananchi wametakiwa kushiriki kwenye mikutano ya kimaendeleo inayohitishwa na viongozi kwenye maeneo yao ili kupanga mikakati mbalimbali ya kimaendeleo
Wito huo umetolewa na afisa mtendaji wa kata ya msasani Julietha Sanga amesema maamuzi yote ya kimaendeleo yanatolewa na wananchi kwa kushirikiana na viongozi wao

afisa mtendaji wa kata ya Msasani Julietha sanga akiongea na mwandishi wa ChaiFm ofisini kwake
sauti ya afisa mtendaji kata ya msasani
Adam Mwenyekiti ni mwenyekiti wa mtaa wa Bulyaga amesema kuna umuhimu wa kushiriki kwenye mikutano ya mitaa,vijiji hadi kata waache kupuuza kwani wananchi ndiyo wenye kuleta maendeleo
sauti ya mwenyekiti wa mtaa
Mariam Igomole ni mkazi wa Tukuyu amesema suala la kushiriki kwenye mikutano inayohitishwa kwenye vijiji au mitaa ni muhimu kwani kunampa mwanachi uelewa kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii
sauti ya mariam Igomole
Naye Derick mwalukasa amesema kwenye mikutano inayoitishwa ndiyo sehemu za kueleza changamoto zinazo wakabili kwenye maeneo yao ili kuweza kupata ufumbuzi wa kuzitatua
sauti Derick mwalukasa