Chai FM

Elimu zaidi yahitajika kutunza vyanzo vya maji

28 February 2025, 6:54 pm

Wakati binadamu hawezi kuishi bila maji hali ni kinyume chake kwayo maji huweza kuendelea kuwepo hata bila uwepo wa binadamu, kwa umuhimu huo wa maji ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha, anatunza, analinda na kuhifadhi vyanzo vya maji.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ilolo wakifuatilia kwa makini elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji (picha na Sabina Martin)

Na Sabina Martin – Rungwe

Serikali inatarajia kuweka mipaka katika hifadhi ya mto katalalifu Kijiji Cha Ilolo wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
Akizungumza katika mkutano wa Kijiji hicho afisa maendeleo ya jamii kutoka bodi ya maji Bonde la ziwa Nyasa Bi. Chiwaya Nkomola amesema wanaendelea kutoa elimu ya kutunza, kuhifadhi na kulinda vyanzo vya maji katika jamii.

Sauti ya Afisa maendeleo ya jamii kutoka bodi ya maji bonde la ziwa nyasa

Aidha Bi.Chiwaya amesema kuwa kabla ya zoezi la uwekaji wa mipaka hiyo walianza kuishirikisha jamii hususani wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu katika hifadhi ya mto Katalalifu.

Sauti ya Bi. Chiwaya

Baadhi ya wananchi wakizungumzq na kituo hiki pembeni ya mkutano huo Bw. Stiven John,.Fred Jumbo, Ndigwako Syete na Aziza Andrea wamesema elimu waliyoipata itawasaidia zaidi katika utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji huku wakiiomba serikali kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi wa maeneo mbalimbali.

Sauti za wananchi wa kijiji cha Ilolo

Kwa kujibu wa Sheria ya mazingira ya Mwaka 2004 hairuhusu mwananchi yeyote kufanya shughuli za kibinadam ndani ya mita 60 kutoka katika chanzo Cha maji.

Pichani ni baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji cha ilolo pamoja na wataalamu kutoka ofisi ya kata, ofisi ya mazingira halmashauri ya Rungwe, RUWASA na wataalamu kutoka bodi ya maji bonde la ziwa nyasa

Ikumbukwe kuwa uwekaji wa mipaka( Bicon) katika maeneo ya hifazi ya vyanzo vya maji husaidia kutunza mazingira na vyanzo hivyo sambamba na upatikanaji wa maji ya uhakika kwa wananchi kwaajili ya matumizi ya sasa na vizazi vijavyo.