Chai FM
Chai FM
27 October 2026, 9:17 pm

kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi ikikagua ujenzi wa kituo cha afya kata ya kinyala [picha na Noah Kibona]
ilikukabiliana na changamoto ya kufuata huduma ya afya umabli mrefu wakazi wa kata ya kinyala wameishukuru serkali kwa kuwajengea kituo cha afya
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi wilayani Rungwe ikiongozwa na Mwenyekiti wa chama ndugu Meckson Mwakipunga imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kujilizisha na utekelezaji wake ikiwa ni pamoja na thamani ya fedha zilizotolewa na serikali
Ikisomwa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya kamati hiyo iliyoandaliwa na mganga mfawidhi wa kituo hicho cha afya Geofrey Sanga kiasi cha shilingi 669,348,538.00 z ilipokelewa kutoka serikali kuu kwaajili ya ujenzi wa kituo hicho
Sauti ya msoma taarifa 1
Hata hiyo amezitaja faida za mradi huo wa kituo cha afya kinyala kwa wakazi wa kata hiyo na maeneo ya jirani kuwa ni kuwazogezea huduma ya matibau pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na changamoto za uzazi kwa kina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga
Sauti ya msoma taarifa 2
Mwakipunga ametumia nafasi hiyo kuishukuru serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inayoongeza na Dr Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwaajili ya kuwapelekea wananchi huduma ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya maeneo mbalimbali ya nchi

Majengo ya kitu cha afya kinyala [Picha na Noah Kibona]
Sauti ya mwenyekiti wa chama cha mapinduzi nd, Meckson Mwakipunga
Naye Diwani wa kata hiyo ya kinyala Hami Chitenga ameIshukuru kamati hiyo ya siasa kwakukagua utekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi vizuri na inayo tekelezwa kwa vitetendo
Aidha amesema pamoja na kupatiwa kituo hicho cha afya licha ya kuwepo kwa maji ameiomba mamlaka ya maji kusogeza huduma hiyo ya maji ili huduma iezweze kuimalika
Sauti ya Diwani wa kata ya kinyala